CHUKUA TAHADHARI MAISHANII

Unaweza kukana kuwa UKIMWI haupo, lakini hilo haitaondoa ukweli kwamba kwa kila dakika mbili zinazo pita kijana mwenye umri kati ya miaka 15-24 anaambukizwa virusi vya UKIMWI katika ulimwengu huu. Hadi mwaka 2016 shirika la afya ulimwenguni lilionesha kuwepo watu 36.7 milion ambao walik

.

 

Unaweza kukana kuwa UKIMWI haupo, lakini hilo haitaondoa ukweli kwamba  kwa kila dakika mbili zinazo pita kijana mwenye umri kati ya miaka 15-24 anaambukizwa virusi vya UKIMWI katika ulimwengu huu. Hadi mwaka 2016 shirika la afya ulimwenguni lilionesha kuwepo watu 36.7 milion   ambao walikuwa na maambukizi ya viusi vya UKIMWI  kati ya hao 25.6 milion waliishi katika bara la afrika. Takwimu hizi zinadhihirisha kuwa katika bara la afrika ndiko yaliko makao makuu ya ugonjwa huu hatari ugonjwa wa UKIMWI. Baadhi ya nchi katika bara hili zinakiwango cha juu cha maambukizi  kiasi kwamba  kwakila watu 100 zaidi ya 20 wanaishi na virusi vya UKIMWI.

Wakati njia za kueneza virusi vya ugonjwa huu zimebaki zile zile, mahusiano ya kimwili (uzinzi na uasherati), mama mjamzito kumwambukiza motto wake, na kuongezwa damu isiyo salama, bado idadi kuwa ya maambukuzi inahusishwa na njia moja tu ya uzinzi na uasherati . Kwa bahati mbaya sana UKIMWI  umegeuka kuwa mradi mzuri na unalipa vizuri. Wakati wengi wanapoteza wapendwa wao, majumba yanafungwa, watoto wanabaki yatima, wajane na wagane wanaongezeka, sambamba na utapia mlo, mashirika ya kimataifa yanamwaga fedha za kutosha katika mradi wa UKIMWI kwa nia njema ya kusaidia jamii hizi, na katika baadhi ya nchi sehemu kubwa huelekeza katika mishahara na marupurupu ya wasio walengwa . Kama hujaguswa na tatizo la UKIMWI yumkini hujafikiria vizuri .

Vijana kati ya miaka 15-24 wanaambukizwa sana kwa sababu ni umri wenye mabadiliko makubwa ya mwili yanayowafanya wengi kuwa limbukeni  na kufuata mkumbo. Wengi wanapoiga tabia bandia na kutupilia mbali tabia zao halisi za nyumbani. Mwisho hujikuta wamenaswa katika tabia hatarishi zinazowatumbukiza katika kuambukizwa virusi. Katika matukio ya mikusanyiko kama sherehe za mwaka mpya, krismas , pasaka, na sherehe zingine za kidini au sherehe za kiserikali,wengi wa vijana wa umri huu hujitumbukiza katika  vitendo vichafu kwa kufuata mkumbo. Chunguza katika mazingra ya kanisa lako au mitaa yako uone mienendo ya vijana wengi wa umri huo, kila takataka ni yao. Wazazi no kwassababu ya masumbufu ya maisha haya na utandawazi , wamesalimu amri kwa watoto wao na kusubiri matokeo ya ajali mbaya watakazo pata vijana wao . Lakini wanappata taarifa kwa vijana wao wana virusi vya UKIMWI  huhamaki na kuanza kuwa fyolea kama hawakujua kuwa mchuma janga hula na wa kwao .

Zamani ilidaniwa kuwa ugonjwa huu ni wa watu wa mjini . Leo hakuna mipaka ya mji na vijijini, Maana wanapatia mjini na kuugulia vijijini ambako pia huwaambukiza wengine. Huwezi kumtambua mwathirika kwa  macho maana wako watu wanaonekana wanene na wenye vitambi, wengine ni waheshimiwa, maofisa, watawala, wachungaji, maaktari, wakulima, matajiri na masikini lakini wameambukizwa. Hadi sasa hakuna dawa iliyafahamika ya kutibu ugonjwa huu zaidi ya dawa ambazo haziponyi ugonjwa huu

Inawezekana kuishi bila maambukizi ya UKIMWI . Tujifunze

Epuka kufuata mkumbo wa majaribio ya kijinga kwenye mwili wako. Kumbuka mwilimwako ni wako , Majaribio yoyote ya uzinzi na uasherati yanakuongezea nafasi na fursa ya kupata VVU/UKIMWI. Familia yako, ndugu, wazazi, rafikizako na jamaa zako wanatamani kukuona ukiendelea kuishi maisha bora ya kutokuwa na VVU/UKIMWI. Kwanini usijitunze?Kijana kama umefikia umri wa kuoa au umria wa kuolewa na umekomaa oa au uolewe kulingana na utaratibu wa kaawaida upate Baraka zote . Achana na njia za mikato, za kufanya majaribio kwanza kwa dhana potofu ya ibilisi kua wote wanajaribu miili kwanza ..

Usinunue ushauri kwa ibilisi

NUNUA USHAURI KWA KRISTO ALIYE KUUMBA ALIYE KUFIA NA AMBAYE SI MUDA MREFU NA KUJA KUKUCHUKUA KWENDA KWA BABA