SABATO NA AFYA YA MWANADAMU

Baada ya kazi ya uumbaji , biblia imeandikwa ‘’basi mbingu a nchi zikamalizika na jeshi lake lote. Na siku ya saba Mungu alimaliza kazi yake yote aliyoifanya Mungu akaibarikia siku ya saba ,akaitakasa kwa sababu katika siku hiyo Mungu alistarehe, akaacha kufanya kazi yake yote aliyoiun

.

 

[Mwanzo 2:3]

Muumbaji alipopumzika siku ya saba ya kwanza baada ya uumbaji ilikuwa siku ya pili tu baada ya kumuumba mwanadamu wa kwanza kwa sura na mfano wake .   Unadhani kwa nini siku ya pili tu baada tu ya kumuumba mwanadamu ndipo tu pumziko la sabato likaingia na MUNGU akapumzika? Pamoja na sababu kuwa mwisho wa juma umewasili ilikuwa ni mpango wa MUNGU mara tu baada ya kumpatia mwanadamu kazi ya kitiisha viumbe na kumwelekeza chakula kifaacho kwa afya yake, kumwekea kielelezo cha kupumzika , kwa afya yake haikumaanisha kuwakatika siku sita kabla ya sabbato Adanu angefanya kazi kama mashine isiyopumzika, La, hasha maana katika siku za juma la uumbaji, Baba, kwa hekima yake alikuwa ameweka mapumziko madogo madogo ya usiku kwa kuweka mwanga mdogo utawale usiku kuashiria kuwa na mapumziko mafupi katikati ya juma kabla ya pumziko lile kubwa mwisho wa juma.

Hakuna mahali popote katika Biblia ambapo panaonesha mabadilik rasmi yaliyofanywa na MUNGU kuondoa pumziko la siku ya saba. Badala yake tunaona maelezo zaidi yanayotoa maelekezo zaidi ya kupumzika siku ya saba ‘’Wana wa Israeli walipokiona wakauliza ni nini hiki? Maana hawakujua ni kitu gani. Musa akawaambia ndio mkate ambao Bwana  amewapa ninyi mle . Neno hili ndilo alilo agiga bwana, okoteni ninyi kitu hicho kila mtu kama ulaji wake ulivyo; kichwa pishi, kama hesabu ya watu wenu ilivyo, ndivyo mtakavyo twaa kila mtu kwaajili ya hao walio hemani mwake. Basi ikawa siku ya sita wakaokota kile chakula sehemu maradufu, kila mtu pishi mbili, na wazee wa mkutano wakaenda kumwambia Musa. Ndilo neon alilolinena Bwana, kesho ni starehe takatifu, Sabato takatifu kwa Bwana; okeni mtakacho oka na kutokosa mtakacho tokosa; na hicho kitakachosalia jiwekeeni kilindwe hata asubuhi, kama Musa alivyowaagiza, nacho hakikutoa ovundo wala kuindia mabuu. Musa akasema, haya, kuleni hiki leo, kwa kuwa leo ni Sabato ya Bwana; leo hamtakiona nje barani.(kutoka16:15-25)’’.

Mungu aliwapa wana  wa Israeli maelekezo ya kudumisha pumziko la siku ya saba wakiwa njiani kuelekea nchi ya ahadi. Hata alipowapa upendeleo wa kula chakula cha malaika, nafaka ya mbiguni waiyookota kila siku sawa na ulaji wa familia, aliwaelekeza kuwa na kiasi, kutookota zaidi katika siku za kawaida na kuokota maradufu katika siku ya maandalio ya sabato, kisha kupumzika siku ya sabato ili kujenga afya zao .

Tunaweza kuondoa mambo machache waliyofanya kujenga afya zao katika  siku ya Sabato.

  1. Walipumzika
  2. Walifanya ibada kwa MUNGU wao
  3. Walikula nakushiba maana walikuwa na chakula cha kutosha familia, mithili ya pumziko la siku ya saba kabla ya dhambi.

Pumziko lile la  Sabato ya  kwanza pale edeni, Adamu alikuwa amezungukwa na vyakula tele vya asili visivyo  hitaji kutokoswa wala kupashwa joto. Vyote vilikuwa na joto la kiwango sahihi kwa afya yake.

 Mungu huyohuyo aliye abudiwa na adamu kule bustsnini edeni ndiye huyo anayeelekeza wanadamu kupumzika siku ya saba kwa afya zao pia. Lakini katika kupumzika huku, kwa kuwa leo hakuna mana inayodondoka ili wanadamu waokote kama ilivyo kuwa wakati wa musa, ikiwa hatuna vifaa vya kuhifadhia chakula kisipoteze joto, Mungu ameelekeza kukipasha joto chakula ili kiwe salama kwa afya zetu ‘’Nawashauri watu wote kula chakula cha joto la uvuguvugu kila asubuhi (Shuhuda za kanisa kitabu cha pili,603, 1870 ), kisiliwe chakula cha moto sana au  cha baridi, Chakula cha baridi sana hakifai kwa afya kwani lazima mwili ukipashe joto kwanza ndipo kiyeyushwe na kufyonzwa . Ndiyo maana maelekezo ya kutunza mwili kiafya kama hekalu la roho mtakatifu kila mmoja anashauriwa kuwa ikiwa chakula kimepoa kipashwe joto kabla ya kuliwa. Mungu alipowaelekeza Israeli kuokota mana mara mbili siku ya maandalio ya sabato alikuwa akiwafundisha wao na sisi  kanuni ya kukamilisha maandalizi yakiwemo ya chakula siku kabla ya sabato ili kubakia huru na shughuli za ibada tu siku ya Sabato. Ndipo linatimia lile fungu lisemalo ‘’siku sita fanya kazi utende mambo yako yote’’. Siku ya sabato ni sherehe ya kumbukumbu ya uumbaji na ukombozi wa mwanadamu. Kwa sababu maalumu tunaweza kufunga, lakini katika ratiba ya kawaida, familia zinashauriwa kuandaa chakula kizuri, cha kutosha, na cha pekee ’’Hebu wale wanao hamasisha matengenezo ya afya watende kama wanvyoongea. Watupilie mbali kila kinachodhuru mwili na kutumia chakula bora na rahisi. Matunda ni bora mno, na huepusha purukushani nyingi na mapishi. Achana na vyakula vya sukari nyingi mfano keki, biscuit, na kitindamlo. Kuliwe aina chache za vyakula kwa kila mlo na kwa moyo wa shukrani (Barua ya 135,1902; CDF 873).Tunapokula kwa ulafi tunaitendea dhambi miili yetu. Siku ya sabato katika nyumba ya MUNGU walafi wataketi na kusinzia licha ya kuwepo mahubiri ya kweli za Mungu zinazochoma mioyo. Hawawezi kukaa macho. Je unadhani watu kama hawa wanamtukuza Mungu katika miili na roho zao? Ambayo ni mali yake? Hapana; Hawamuheshimu (CDF 136.4 ).

Tusiandae aina nyingi za vyakula siku ya Sabato kinatakiwa kuwa rahisi, na ulaji wa mtu unatakiwa kuwa kidogo ili akili iwe safi na makini kutafakari mambo ya kiroho. Tumbo likifura na ubongo unafura pia. Unaweza kusikia ujumbe wa thamani kubwa lakini usiutilie maanani kwa sababu akili imechanganyikiwa na ulaji usio na kiasi, kwa kula kupita kiasi siku ya sabato wengi hutenda zaidi ya wanavyo fikiri, kwa kutojistahirisha kupokea faida zitokanazo na fursa takatifu (huduma ya uponyaji Uk 307, 1905 ).

Yako maelezo ya kutosha juu ya chakula na Sabato kwa afya ya mwanadamu. Kama vile sabato ilivyo takatifu, tunapokuja kumwabudu Mungu mtakatifu miili yetu hii anayotaka tuitoe kwake kikamilifu kuwa dhabihu iliyosafi, takatifu yakumpendeza yeye yapaswa kuwa katika hali nzuri ya kumpokea. Saato ilifanyika kwaajili ya mwanadamu na si mwanadamu kwaajili ya sabato Pumziko la sabato lilikusudiwa kumpa mwanadamu Tafakari ya ukuu wa Muumbaji wake na jinsi tulivyo kombolewa kisha tujitoe kwake mara dufu.

Andaa chakula chako, mavazi yako, moyo wako, zaka na sadaka zako, kwaajili ya kukutana na mkombozi wako siku ya SABATO, Kamwe usiruhusu kitu chochote kichukuwe muda wako au kukukosesha kukutana na Mungu wako katika Ibada ya sabato. Kumbuka kwamba Siku sita fanya kazi utende mambo yako yote lakini siki ya saba ni sabato ya Bwana Mungu wako siku hiyo usifanye kazi yoyote………………………………………… (kutoka 20:8-11)