Mambo muhimu ya kuzingatia katika ulaji ili kuifanya afya yako iwe vizuri kila wakati.

Comments · 646 Views

Afya ni jambo muhimu sana kwakila mtu, ni jambo ambalo kila mwanadamu analihitaji na kulitafuta kwa udi na uvumba.

Ukiwa na afya njema utakuwa umefanikiwa katika mambo mengi sana utaweza kufanya kila kitu katika maisha yako endapo utakuwa na afya njema.

Kumekuwa na matati

Moja kati ya matokeo ya kuwa na afya mbovu ni pamoja na kupoteza pesa nying kwa sababu ya kutafuta matibabu, kuacha watoto wakiwa ni yatima kwa sababu ya vifo lakini pia nguvu ya taifa kupotea kwa sababu ya kuwa na afya mbovu

Kumbuka kuwa kwa asilimia kubwa ya magonjwa ambayo yamekuwa yakisumbua watu wengi leo yamesababishwa na mfumo na mitindo mibovu ya maisha yetu ambayo inatupelekea kupata matatizo ya kiafya mfano magonjwa ya moyo nk.

Vyakula ambavyo vimekuwa vikitumika kwa sehemu kubwa ni vyakula vyenye madhara makubwa na vyenye kutaharisha afya, ni kweli kwamba kila mwanadamu mwenye akili timamu anafahamu hili kuwa kama chakula anacho kila kinaweza kumsababishia kuwa na afya njema au kumuharibia kabisa maisha yake kwa kuifanya afya kuwa katika hali ya matatizo makubwa.

Kama watu wakibadili mitindo ya maisha yao na kufanya maisha yao kuwa tofauti kwa kuzingatia kanuni za ulaji na kanuni za afya ndipo mabadiliko makubwa yatakapo tokea katika afya ya kila nmwanadamu hivyo kukusaidia kuepuka magonjwa yasiyo ya lazima.

Habari njema ni kwamba  unaweza kuifanya afya yako kuwa vizuri nakuepuka magonjwa yasiyo ya lazima kwa kufanya na kufuata kanuni za afya katika suala zima la ulaji ambazo kama mtu akifuata kwa uaminifu kanuni hizo hatojuta kamwe

Kwa bahati iliyombaya zaidi watazania na waafrika wengi sana wamejikuta wakitumia yakula ambavyo havina faida yoyote katika afya zao lakini kusababishia afya zao kuingia katika matatizo makubwa sana na kwa sababu ya ujinga watu wamekuwa wakitumia vitu vyenye madhara wakidhani kuwa ni ufahali na bila kujua vitu hvyo vinamadhara makubwa katika afya zao wamekuwa wakilipia kwa gharama kubwa vitu hivo.

Katika makala haya leo, niakuonesha mambo ya msingi ya kuzingatia katika suala la ulaji ili kufanya afya yako iwe vizuri.

  1. Acha kula/kutumia vya kula viloivyo kobolewa.

Kimsingi vyakula vilivyo kobolewa havina faida yoyote katika afya yako mfano sembe unapo kuwa unatumia vyakula vyote vilivyo kobolewa mfano sembe hauongezi virutubisho vyovyote katika afya yako kwa sabatu ni sawasawa na kula makapi. Kumbuka kwamba makapi hayana faida yoyote katika mwili wa binadamu.

Kwa bahati iliyo mbaya watu wengi leo wamejikuta wakichukua vyakula vyenye faida katika miili yao na kuwapatia wanyama na ndege wa kufugwa watu wanakoboa mahindi kisha wanachukua pumba na kwenda kuwapa nguruwe, sungura na kuku wakati huo yeye anatumia makapi tuu.

  1. Acha kutumia soda.

Vinywaji hivi havina faida yoyote katika afya yako zaidi ya hasara mfano utumiaji wa soda kama cokacola, kinywaji hiki kinatengenezwa kwa kemikali nyingi ambazo ni lazima mwisho wa siku kitakuletea madhara makibwa katika afya imesikika kuwa inawekwa sukuri yenye ujazo wa vijiko tisa [9] ambayo siku moja itasababisha madhara yasiyokuwa na sababu katika afya yako.

Na badala ya soda unashauriwa kutumia maji mengi kila siku kitu ambacho kinafaida kubwa sana katika afya yako.

Madaktari wakuba duniani na wana sayansi wanasema kuwa sehemu kubwa ya mwili wa mwanadamu yanatakiwa kuwepo maji sio soda kulingana na kemikali zinazowekwa kwatika soda unahimizwa kuacha kabisa matumizi ya soda badala yake unaweza kutengeneza juisi za matunda mbalimbali za matunda hizo ndizo zitakusaidia.

  1. Acha kutumia/kuvuta sigara.

Kutumia siagara mwisho wa siku kunaenda uharibu mfumo mzima wa upumuaji katika mwili wako kitendo hicho huathiri na kuchafua mapafu na pia kuvuta sigara kunaweza kukufanya ukaumwa kifua kikuu kimsingi uvutaji wa sigara ni hatari kwa afya yako kama ulikuwa ukivuta sigara unashauriwa kuacha kitendo hicho maramoja.

  1. Acha kutumia mafuta ya wanyama.

Mafuta mengi ambayo yanatengenezwa kwa kupitia wanyama mbali mbali yanamadhara makubwa sana katika afya yako mfano mafuta ya korie.

Mafuta hayo huziba baadhi ya mishipa ya damu mwilini hivyo kusababisha matatizo mengine kama matatizo ya moyo.

Mbadala wa mafuta hayo unashauriwa kutumia mafuta ya mimea kama alizeti mafuta hayo hayana shida katika afya ya mwanadamu yanafaida kubwa sana katika afya yako.

  1. Acha kutumia na kula nyama nyekundu.

Ukiangalia kwa umakini kmadhara ya utumiaji wa nyama hasa nyama nyekundu unaweza ukashangaa sana na kuogopa lakini kwa ufupi hupaswi kutumia nyama hasa nyama nyekundu katika mwili wako mfano; mbuzi, kondoo, ng’ombe.

Badala yake unashauriwa kula nyama nyeupe kama nyama ya kuku, samaki nahata dagaa

Lakini pia kuna baadhi ya mimea ambayo inatoa virutubisho kama vile vyinavyo patikana kwenye nyama unaweza kutumia hivyo mfano soya inafaida kubwa sana katika afya yako.

  1. Acha kutumia na kula vyakula vya baridi.

Unapokuwa unakula vyakula vya baridi unafanya mashine za mwili kutafuta joto laziada ili kukipasha chakula kipate joto ambalo litaendana na lile joto la mwili na hivyo kusababisha  mfumo wa mmeng’enyo  kuchelewa kumeng’enya chakula kwa wakati unao takiwa; madhara mengineyo ambayo yanaweza kupatikana kwa kutumia vyakula vya baridi ni pamoja na vidonda ya tumbo.

Nyongeza/ zawadi

Mazoezi pia yana umuhimu mkubwa sana katika afya yako unashauriwa kufanya mazoezi kila siki ikibidi kila asubuhi na jioni kwa muda wa dakika 30-45 thelathini mpaka dakikan arobaini na tano.

Hayo hapo juu ni baadhi tu ya mambo ambayo unapaswa kizingatia katika suala la ulaji ili kuifanya afya yako iwe bora